Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
DOI:
https://doi.org/10.47941/ejl.2783Keywords:
Viwakilishi vya kijinsia, Usahihi wa uhawilishaji, Tafsiri, Lugha lengwa, Hadharia lengwa.Abstract
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza na kubainisha usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia kutoka kiswahili lugha isiyo na viwakilishi bainifu vya jinsia kwenda kiingereza lugha yenye viwakilishi bainifu ya jinsia.
Mbinu: Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: Siku Njema ya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Day iliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalaba iliyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza Unmarked Grave iliyotafsiriwa na Githiora (2017). Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natala iliyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza Natala iliyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011). Tamthilia ya Kinjekitile iliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitile iliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Skopos na Nadharia ya Usawa wa Kidhima. Nadharia ya Skopos iliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1978) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo. Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri. Baada ya kubainisha uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duara kutathimini usahihi uhawilishaji huo.
Matokeo: Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiri wa vitabu teule wamehawilisha viwakilishi vya jinsia kwa usahihi na uhawilishaji mwingine ukazua utata. Uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia huwa na athari asi na chanya kwa hadhira lengwa. Mchango wa kipekee kwa nadharia, vitendo na sera: Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi kufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.
Downloads
References
Buljan, Gabrijela, Gradecak-Erdeljic, Tanja (2013). English Morphosyntax on Nouns, Determiners and Pronouns. Osijek: Filozofski fakultet.
Githiora, C. (2017) An Unmarked Grave: A Story of the Mau Mau War. Phonex Publishers.
Halliday, M. (2000). An Introduction to Functional Grammer. Beijing: Foreign Language Teaching and Research Press.
Hussein, E. (1970). Kinjeketile. Oxford University Press: Nairobi. (English).
Hussein, E. (1969). Kinjeketile. Oxford University Press: Nairobi. (Kiswahili).
Kareithi, P. (1969). Kaburi bila Msalaba: Hadithi ya vita vya Mau Mau. Nairobi: East African Publishing House.
Kasu, K. na Marami (2011). Natala. Nairobi. Marimba Publications Ltd.
Kennison, S. & Trofe, J. (2003). Comprehending Pronouns: A role for Word-specific Gender Stereotype Information. Journal of Psycholinguistics Research, 32: 355 – 378.
Khalilova, L. R. (2023). Lexical Gender in Written Business English: A Corpus-Based Approach. Golden BRAIN, 1(4), 196–199. Retrieved from https://researchedu.org/index.php/goldenbrain/article/view/1630. Ilisomwa 15/11/2024
Khan, N. (2019). Case Study as a Method of Qualitative Research in Qualitative Techniques for Workplace Data Analysis (Kur. 170 – 196).
Kimutai, K. (2016). Ulinganifu wa Taarifa za Habari: Tathmini ya Tafsiri kutoka Kiswahili hadi Kipsigis katika kituo cha Kitwek. M.A Thesis University of Nairobi (Haijachapishwa).
Kweyu, D. na Kawegere, F. (2017). A Good Day. Longhorn Publishers.
Mberia, K. (1997). Natala. Nairobi. Marimba Publications Ltd.
Munday, J. (2001). Introducing Translation Studies, Theories and Applications. London: London and New York.
Ngesu, S., Malangwa, P. & Kandagor, M. (2019). “Tathmini ya Mikakati ya Tafsiri ya Vinay na Darbelnet (2004) katika tafsiri ya A Good Day (2019).” Jarida la Mwanga wa Lugha, Juz. 4(1): 129 – 152.
Nida, E. (1964). Towards a Science of Translating: With Special Reference to Principles and Procedures Involved in Bible translating. Leiden: Brill.
Riazi, A. (2018). “Mixed Methods Approaches to Studying Second Language Writing”. The TESOL Encylopedia of English Language Teaching, Juz. 10: 1-6.
Schaffner, C. (1988). Skopos Theory. In M. Baker (ed.) Routledge Encyclopedia of Translation Studies. London: Routledge, pp 235 – 238.
Venuti, L. (2000). The Translation Studies Reader. London and New York, Routledge.
Vermeer, H. (1989). Skopos and commission in translational action. In Chesterman, A. (ed.). Readings in translation theory. pp.173-187.
Walibora, K. (1996). Siku Njema. Nairobi: Longhorn.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
License
Copyright (c) 2025 Mutisya Cosmas Mbithi, Dr. Sarah Ndanu Ngesu, Dr. Esther N. Chomba

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors retain copyright and grant the journal right of first publication with the work simultaneously licensed under a Creative Commons Attribution (CC-BY) 4.0 License that allows others to share the work with an acknowledgment of the work's authorship and initial publication in this journal.