Usawiri wa Wahusika wa Kiume katika Riwaya ya Chozi La Heri
DOI:
https://doi.org/10.47941/ejl.2879Keywords:
Usawiri, Wahusika, Uhalisia, Jinsia, Nadharia, Fasihi.Abstract
Makala hii imechunguza, usawiri wa wahusika wa kume katika riwaya ya Chozi la Heri (2017). Katika ulimwengu wa riwaya ya Kiswahili na fasihi, imekuwa kama jambo la kawaida kuona watafiti wengi wakichunguza masuala ya wanawake zaidi kuliko masuala ya wanaume. Jambo hili limetokana na ukweli kwamba, wanawake wamekuwa wakipiganiwa haki zao ili kuwafanya sawa na wanaume katika nyanja mbalimbali za maisha. Atieno (2019) anaeleza kuwa, kupuuzwa kwa jinsia ya kiume kumechangia hali yao ya upweke, kwani hakuna anayewafikiria wala kuwatetea kama inavyofanyiwa jinsia ya kike. Riwaya hii imeteuliwa kimakusudi kwa sababu inamsawiri mhusika wa kiume katika nyanja mbalimbali za maisha. Makala hii iliogozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inadai kwamba, fasihi inatakiwa kutoa picha halisi ya jamii husika. Nadharia hii ilizuka huko Ulaya katika karne ya kumi na tisa. Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo riwaya ya Chozi la Heri ilisomwa na kuhakikiwa. Ni matumaini yetu kuwa, Makala hii imetoa mwanga mkubwa kuhusiana na masuala ya jinsia ya kiume. Aidha, Makala hii itakuwa kichocheo cha watafiti wa baadaye wa fasihi kuchunguza masuala yanayohusu jinsia ya kiume.
Downloads
References
Atieno, J. (2019). “Utambulisho wa jinsia katika Maumbile si Huja na Paradiso.” Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)
Bayyo, F. (2020). “Usawiri wa jinsi ya kiume katika riwaya teule za Shafi Adam Shafi.” Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Dodoma. (Haijachapishwa)
Lukacs, G. (1972). Studies in European Realism. The Universal Library GROSSET $DUNLAP, NEW YORK.
Matei, A. (2017). Chozi la Heri. Nairobi, Kenya.
Mlacha, S. (1985) “Wahusika katika riwaya ya Kiswahili (1970-1982)”, Katika jarida la Mulika, Toleo la 17, Uk. 29-44, Dar es salaam, TUKI.
Mohammed, K. (2018). “Kuchunguza usawiri wa mhusika mwanamme katika riwaya ya Kiswahili: Joka la mdimu na Watoto wa Mama N’tilie. “Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu huria cha Tanzania. (Haijachapishwa)
Mulokozi, M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Kauttu publishers.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
License
Copyright (c) 2025 Agnes Mwongeli Kiema, Dr. John Mutua, Dr. Sarah Ndanu Ngesu

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors retain copyright and grant the journal right of first publication with the work simultaneously licensed under a Creative Commons Attribution (CC-BY) 4.0 License that allows others to share the work with an acknowledgment of the work's authorship and initial publication in this journal.