Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili
DOI:
https://doi.org/10.47941/ejl.2936Keywords:
Usawiri, Wahusika, Uchanganuzu, Ulinganishi, MtazamoAbstract
Makala haya yanakusudia kuchanganua na kulinganisha wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili ambazo ni: Mwisho wa Kosa, (1987) iliyoandikwa na Zainabu Burhani, Siku Njema (1996), iliyoandikwa na Ken Walibora, Taswira za Mawingu, (2011) iliyoandikwa na Sinjiri Mukuba na Nguu za Jadi, (2021) iliyoandikwa na Clara Momanyi. Makala haya yanaegemea nadharia ya Mwanamume Mpya. Nadharia hii iliasisiwa na Beynon (2002). Nadharia ya Mwanamume Mpya inajaribu kueleza kwa nini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila kuonesha tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Mihimili ya nadharia ya Mwanamume Mpya iliyoongoza makala haya ni kusaidia wake zao na wanawake wengine katika jamii kujiendeleza kielimu na kikazi, kukubali majukumu yoyote ya kiuana bila kujali jinsia au watu wanaomzunguka, kutoonesha udikteta katika familia zao pamoja na jamii inayowazunguka, kuwaona wanawake kama viumbe sawa na wanaume kwa kuwaheshimu na kuwapenda katika kila nyanja wanazokuwepo na kukosoa nafsi zao na mazoea yao kama wanaume. Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha na kulinganua usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule. Data iliyotumika katika Makala haya ilitolewa maktabani. Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu. Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa kiume. Kwa hivyo, kulingana na waandishi wa kike mwanamume ni mpya. Kulingana na mpito wa wakati waandishi wa karne ya ishirini wamemsawiri mhusika wa kiume kwa mitazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa karne ya ishirini na moja. Kwa hivyo mwanamume ni mpya kulingana na waandishi wa karne ya ishirini.
Downloads
References
Badru, Z. (2019). “Mfumo Dume- Chanzo cha Ufungwa wa Mwanamume: Uhakiki
wa Semi Kutoka Jamii za Kiafrika.” Chuo Kikuu cha Dodoma. (Haijachapishwa)
Beynon, J. (2002). Masculinity and Culture. Philadelphia, Open University Press. Bly, R. (1990). Iron John: A Book about Men. New York: Minesota Publishers Ltd.
Burhani, Z. (1987). Mwisho wa Kosa. Nairobi: Longhorn Kenya
Hamisi, L. (2018). The Boy Child and New Gender Imperatives in Kenya: Investigating School Dropout among Boys in Marakwet County.
Kobia, J. (2008). “Taswira za Kiuana katika Nyimbo za Tohara za Wanaume Miongoni mwa Waigembe.” Tasnifu ya Shahada ya Uzamifu katika Fasihi ya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa).
Ligaga, D. (2020). Women, Visibility and Morality in Kenyan Popular Media. Grahamstown: NISC (pty) Ltd.
Matandura, B. (2007). “Taswira Dumifu za Uana katika Fasihi ya Kiswahili ya Watoto” M.A Thesis University of Nairobi
Mapunjo, G. (2014). “Usawiri wa Mwanamke kama Kiongozi katika Tamthiliya: Uchunguzi wa Kivuli Kinaishi na Nguzo Mama,” Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa)
Ministry of Education, Science and Technology, (2014). Free Secondary Education Policy in Kenya.
Mirikau, S. (2011). “Tasnifu ya Mwanamke katika Tamthilia za Wamitila” Tasnifu ya Shahada ya Uzamili Chuo Kikuu cha Nairobi.
Momanyi, C. (2021). Nguu za Jadi. Nairobi vide-muwa
Morell, R. (2002). “Mutations in a Novel Genre Are Associated with Hearing Loss, Linked to the DFNB 6. Locus vol.7
Mosha, D. (2019). Ulinganishaji wa Majukumu ya Wahusika Kijinsia katika Nyimbo za Watoto na Uhalisia Wake katika Malezi ya Watoto Nchini Tanzania. Tasnifu ya Uzamivu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Haijachapishwa).
Mukuba, S. (2011). Taswira za Mawingu. Nairobi: Moran Publishers
Muniu, G. (2011). Ujagina wa Mwanamke katika Pango. Tasnifu ya Chuo Kikuu cha Nairobi.
Ndungwa, B. (2012). “The Challenges of Akamba Single Mothers in References to Parenting the Boy Child in the Light of Chistian Complementary Feminism.” M.A Thesis University of Nairobi.
Newman, M. (2012). Community Food Webs Data and Theoty, USA, International Union for Conservation of Nature, University of Arizona.
Nzong’a, P. (2020).” Mgao Mpya wa Kazi za Mwanaume katika Hadithi Fupi za Kiswahili” Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
Walibora, K. (1996). Siku Njema. Nairobi: Longhorn Publishers
Wamitila, K. W. (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi, Nairobi: Vide-Muwa Publishers.
Yego, E. (2013). “Nafasi ya Mwanamke: Jinsi Anavyotetewa katika Nyimbo za Taarab za Zanzibar” Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapisha)
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
License
Copyright (c) 2025 Dorcas Kasiva Kimondiu, Dr. Francis Musyoka , Dr. Esther Chomba

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
Authors retain copyright and grant the journal right of first publication with the work simultaneously licensed under a Creative Commons Attribution (CC-BY) 4.0 License that allows others to share the work with an acknowledgment of the work's authorship and initial publication in this journal.